Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-IRAQ-IS-Marekani-Mapigano-Usalama

Kobane: mashambulizi ya muungano dhidi ya IS yaanza kuzaa matunda

Wapiganaji wa Dola la Kiislam wameukaribia mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Wapiganaji hao wanadhibiti sehemu kubwa ya mkoa wa Al-Ambar, na wameanza kutekeleza mashambulizi katika baadhi ya maeneo ya mji wa Iraq unaokaliwa na watu wengi kutoka jamii ya Washia.

Mashambulizi ya muungano dhidi ya IS yanaendelea katika mji wa Kobane.
Mashambulizi ya muungano dhidi ya IS yanaendelea katika mji wa Kobane. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya Jumanne wiki hii ni 25.

Wakuu wa kijeshi wa muungano, waliokutana Jumanne wiki hii mjini Washington wamesema kinacho hitajika wakati huu ni mshikamano kati ya majeshi ya mataifa yanayoshiriki vita dhidi ya wapiganaji wa Doal la kiislam.

Wakati huphuo jeshi la Marekani linaendelea na mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam pembezuni mwa mji wa Kobane nchini Syria kwenye mpaka wa Uturuki. Mashambulizi hayo yanaonekana kuzaa matunda.

Majeshi ya muungano yamezidisha mashambulizi katika siku za hivi karibuni, ambapo Kobane inashuhudia kwa siku ya thelathini mapambano kati ya majeshi hayo ya muungano na wapiganaji wa Dola la Kiislam. Tangu Jumatatu hadi Jumanne wiki hii, majeshi ya muungano wa kimataifa yameendesha mashambulizi zaidi ya 22.

Ni mapema mno kusema kuthibitisha kwamba wapiganaji wqa Dola la Kiislam wameanza kupoteza nguvu katika mjini wa Kobane, lakini kwa mujibu wa habari tulizopewa na wapiganaji wa kikurdi pamoja na wakimbizi wa Kobane, ambapo wapiganaji wa Dola la Kiislam wameonekana kuwa na nguvu katika saa 48 zilizopita hasa katika maeneo wanayodhibiti yaliyo kando na mji wa Kobane>

“ Kwa muda wa siku mbili zilizopita tumekuwa tumekataa tamaa, lakini tangu Jumatatu tumeanza kuwa na matumaini”, wamesema wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.