Canada: mashambulizi katika mji wa Ottawa
Michael Zehaf-Bibeau, mwenye umri wa miaka 32 aliuawa Jumatano Oktoba 22 na vikosi vya usalama wakati alipokua akijaribu kuingia ndani ya jengo la Bunge mjini Ottawa nchini Canada akiwa na silaha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hali hiyo ilizua wasiwasi, baada ya kusikika milio mingi ya risase ndani ya jengo hilo na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.
Inasadikiwa kua mtu huyo ana uhusiano na Martin Rouleau, aliye endesha shambulio Jumatano Oktoba 20 dhidi ya wanajeshi wawili mjini Québec. Hakuna kundi ambalo limedai kutekeleza mashambulizi hayo. Lakini viongozi wa Canada wana amini kwamba ni mashambulizi ya kigaidi.
Mashambulizi hayo yanatokea wakati ambapo Canada iliwatuma wanajeshi wake kushiriki katika muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Hata hivo, Stephen Harper, amesema Canada haitishiki na vitisho hivyo, na itaendelea na vita dhidi ya ugaidi hususan Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Michael Zehaf-Bibeau, ni mkaazi wa Montréal, na amekua akifahamika na vyombo vya sheria kutokana na uhalifu aliyokua akitekeleza katika miji ya Québec na Vancouver,