Pata taarifa kuu
MAREKANI-FERGUSON-MAANDAMANO-Usalama

Marekani: hali ya tahadhari yatangazwa Ferguson

Mkuu wa jimbo la Missouri ametangaza hali ya tahadhari na kuagiza kutumwa kwa askari polisi na wanajeshi katika mji wa Ferguson, eneo liliyo kaskazini mashariki mwa mji wa St. Louis County, kwa muda wa siku 30.

Maandamano dhidi ya kifo cha Michael Brown, katika mji wa Missouri, Novemba 17 mwaka 2014, Marekani.
Maandamano dhidi ya kifo cha Michael Brown, katika mji wa Missouri, Novemba 17 mwaka 2014, Marekani. REUTERS/Jim Young
Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyo wa jimbo la Missouri ana hofu ya kutokea kwa machafuko makubwa, wakati ambapo jopu la wachunguzi linatazamiwa kukamilisha hivi karibuni uchunguzi wao, na kuamua iwapo askari polisi mzungu aliye husika katika kifo cha kijana mweusi mwezi Agosti atafuatiliwa na vyombo vya sheria au la.

" Vurugu hazitavumiliwa", ameonya mkuu wa jimbo la Missouri, Jay Nixon. Kwa wakati huu Jay Nixon amechukua uamzi wa kuwatuma askari polisi na wanajeshi katika mji wa Ferguson ili kuimarisha hali ya usalam katika mji huo. Jay Nixon anataka kuzuia maandamano yenye msingi wa kibaguzi yasirudi kutokea kama yale ya mwezi Agosti, baada ya wimbi la machafuko liliyosababisha kifo cha Michael Brown, aliyeuawa kwa risasi sita ziliyofyatuliwa na afisa wa polisi mzungu, Darren Wilson.

Idara ya ujasusi ya Marekani, FBI imechapisha taarifa ambayo inaonya uwezekano wa kutokea kwa vurugu, si tu katika mji Ferguson, lakini nchini kote. Hata hivyo maandamano yamepangwa kufanyika katika miji ya Chicago, Atlanta, Washington baada tu ya kutangazwa matokeo ya jopu la wachunguzi. Jopu hili litaamua katika siku zijazo kama Darren Wilson alijihami, au kama atahukumiwa.

Jumatatu Novemba 17 waandamanaji walizuia kwa muda wa saa moja njia panda katikati ya mji wa St. Louis County. Lakini wanamgambo wa vuguvugu lenye msingi wa kibaguzi la mrengo wa kulia, Ku Kux Klan, lilisambaza vipeperushi na kutishia kutumia silaha dhidi ya waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.