Pata taarifa kuu
HAITI-MARTELLY-MAANDAMANO-SIASA

Waandamanaji wamtaka Michel Martelly ajiuzulu

Hali ya wasiwasi inaendelea kushuhudiwa nchini Haiti. Siku sita baada ya kujiuzulu kwa Waziri mkuu wa nchi hiyo, Laurent Lamothe, rais hajateua mtu yeyote kwenye wadhifa huo.

Maandamano ya kumtaka rais wa Haiti Michel Martelly ajiuzulu, katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Desemba 16 mwaka.
Maandamano ya kumtaka rais wa Haiti Michel Martelly ajiuzulu, katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Desemba 16 mwaka. AFP/Hector Retamal
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Haiti, Michel Martelly ameanzisha mazungumzo na vyama mbalimbali, lakini wapinzani wake wenye msimamo mkali wamekata katu katu mazungumzo hayo, na wameendelea na maandamano wakimtaka rais huyo ajiuzulu.

Katika mji mkuu wa Port-au-Prince, mamia kwa maelfu ya raia wamefurika barabarani, wakimtaka rais Michel Martelly ajiuzulu.

Assad Volcy, mmoja kati ya viongozi wa harakati amefutilia mbali mazungumzo na rais.

Kundi la wafuasi wa vyama vya upinzani ambao wamejiita kwa jina la " Watoto wa Dessalines", limepata mwaliko wa Michel Joseph Martelly kwa ajili ya mkutano Ijumaa Desemba 19 kama sehemu ya mpango wake wa kuondokana na mgogoro huo, limesema kundi hilo.

Kundi hilo la wafuasi wa vyama vya upinzani, limebaini kwamba limechukua uamuzi wa kukataa mwaliko kwa sababu muda umepita kiasi kwa kuzungumza na Michel Martelly.

Watu, ambao ni watoto wa Dessalines wako mitaani. Wana madai yao : " kuondoka kwa Michel Martelly. Ufumbuzi wa mgogoro utapatikana kwa kuondoka madarakani kwa Michel Martelly, kwa sababu pamoja naye, hakutakuwa na uchaguzi wa huru, wa wazi na wa kidemokrasia nchini Haiti", limeendela kusema kundi hilo.

Wakati waandamanaji walipokua wakiandamana katika eneo la mji mkuu, rais Michel Martelly amekua akikukutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vyenye msimamo wa wastani, lakini bado hajatangaza uteuzi wa mtu atakaye chukua nafasi ya Waziri Mkuu aliye jiuzulu, Laurent Lamothe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.