Pata taarifa kuu
MAREKANI-KODI-JAMII

Obama atazamiwa kutangaza ongezeko la kodi kwa matajiri

Barack Obama anatazamiwa kutangaza leo Jumanne Januari 20 saa tatu usiku (saa za Washington ) katika hotuba yake ya kila mwaka mwaka kuhusu hali ya Muungano, ambayo inaweka mfumo wa sera za Marekani kwa mwaka ujao.

Rais Barack Obama, januari 16 mwaka 2015 akiwa Ikulu, washington.
Rais Barack Obama, januari 16 mwaka 2015 akiwa Ikulu, washington. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo inatokea wakati uchumi nchini Marekani unaendelea kudorora, huku ukosefu wa ajira ukiendelea kushuhudiwa, katika kiwango cha asilimia 5.5, ukuaji umepanda (asilimia 5 katika kipindi cha hivi karibuni) na bei ya mafuta imeshuka kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI mjini Washington, Anne-Marie Capomaccio, Barack Obama anaandaa kutoa hotuba yake kuhusu hali ya Muungano kabla yakuondoka madarakani. Rais wa Marekani anataka kufunga ukurasa wa mdororo wa uchumi katika mazingira ya matumaini ya kipekee kwa miaka kumi au kumi na tano.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Washington, Obama atashinikiza faida yake ya sasa na kupendekeza mageuzi kabambe ya kiuchumi.

Baadhi ya maelezo ya mradi huu tayari yametolewa, na mara moja yamewaghadhabisha wajumbe wa chama cha Republican.

Hali hio inahusu suala la mageuzi ya kodi, ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko kwa familia za kitajiri, hasa kwa kuondolewa kwa kodi isiyoeleweka kwa ajili ya kupeleka fedha katika urithi, na kupitia ongezeka la kiwango cha kodi ya mtaji na faida. Ni kusema kuwa asilimia 1 pekee ya familia za raia wa Marekani wanahusika na ongezeko hilo la kodi. Familia ambazo mapato yao yako juu kwa zaidi ya dola milioni 2 kwa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.