Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-DIPLOMASIA

Wanawake 2 katika mazungumzo kati ya Marekani na Cuba

Mazungumzo juu ya kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba yanaanza rasmi leo Alhamisi Janurai 21 katika mjimkuu wa Cuba Havana.

Upande wa Cuba, mwanadiplomasia Josefina Vidal, ambaye ni msimamizi wa mazungumzo na mwenzake wa Marekani, Roberta Jacobson.
Upande wa Cuba, mwanadiplomasia Josefina Vidal, ambaye ni msimamizi wa mazungumzo na mwenzake wa Marekani, Roberta Jacobson. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza katika miaka 35, mwakilishi wa Idara ya Marekani, Roberta Jacobson, anaehusika na masuala ya mataifa ya magharibi, amewasili nchini Cuba kushiriki mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Havana, Véronique Gaymard, Roberta Jacobson aliwasili Jumatano, Januari 21 katika mji wa Havana.

Naibu Katibu dola anehusika na masuala ya Marekani, ni afisa wa ngazi ya juu nchini Marekani kuwasili Cuba tangu mwaka 1980.

Hii ni ziara ya kihistoria ambayo inaanza, wiki tano baada ya tangazo la pamoja lililotolewa na marais Barack Obama na Raul Castro juu ya kufufua mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na kuachiliwa huru kwa wafungwa husika. Mahusiano yaliyovunjika tangu mwaka 1961, pamoja na miaka hamsini ya uadui na vikwazo ambayo Marekani imeendelea kuichukulia Cuba.

Roberta Jacobson atashirikiana katika mazungumzo hayo kwa upande wa Cuba na mwanamke mwingine, Josefina Vidal, ambaye ametokea kuwa moja wa wataalam bora nchini Cuba katika siasa za Marekani na Umoja wa Mataifa, (mtu mwenye hekima) kama alivyomsifu siku moja rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro.

Josefina Vidal ni mwanadiplomasia wa muda mrefu, ambae alihudumu miaka mingi katika kitengo cha maslahi ya raia wa Cuba Washington. Majukumu hayo yalimpelekea kuanzisha mawasiliano yenye thamani katika sehemu za kisiasa na kitaaluma.

Mwaka 2013, wakati wa hotuba yake katika chuo kikuu cha Columbia mjini New York, Josefina Vidal alitolea wito Marekani kufikiria upya sera zake kwa Cuba.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo, Cuba imebadilika zaidi katika miaka mitatu iliyopita ikilinganishwa na miongo miwili iliyopita. Wale wanaomfahamu, upande wa Marekani, wamepongeza taaluma yake.

Wajumbe hao kutoa pande hizo mbili wanafahamiana tangu kitambo, na hali hio huenda ikarahisisha mazungumzo hayo. Jarida liitwalo Miami Herald limebaini kwamba " Wawili hao wana sifa nzuri" na kuthibitisha kwamba " wanawake ni wazungumzaji wazuri".

Majadiliano yanapaswa kuzingatia utaratibu na ratiba ya kuanza kwa mahusiano ya kidiplomasia na ufunguzi wa balozi. Ufunguzi wa balozi za nchi hizo utapewa kipaumbele katika agenda ya mazungumzo ya leo kati ya mjube wa Marekani Jacobson na mjumbe wa Cuba Josefina Vidal. Washington imeomba kuwepo uhuru wa kuingia na kutoka kwa raia wa Cuba katika majengo yake ya ubalozi, kama inavyotakiwa na mikataba, pamoja na uwezekano wa kuteua timu ya wafanyakazi wake, na hakuna kizuizi juu ya idadi ya wanadiplomasia, ambao pia wanatakiwa kupewa uhuru wa kutembea nchini Cuba.

Marekani imejikubalisha kutekeleza yote hayo kwa wafanyakazi wa Cuba watakaotumwa kwenye ubalozi wake Marekani, kama alivyoarifu mwandishi wa RFI Washington, Anne-Marie Capomaccio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.