Pata taarifa kuu
MAREKANI-IS-UGAIDI-USALAMA

John Kerry atuhumiwa kupuuzia athari ya ugaidi

Taarifa mbili ziliyotolea na vmaafisa waandamizi katika utawala wa Obama zimezua mvutano na kukosolewa na Wawakilishi wa raia nchini Marekani.

Askari poli wa jimbo akitoa ulinzi mbele ya mahakama ya Broooklyn, Februari 25 mwaka 2015.
Askari poli wa jimbo akitoa ulinzi mbele ya mahakama ya Broooklyn, Februari 25 mwaka 2015. REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao muhimu katika utawala wa Obama walitoa hivi karibuni taarifa zinazotofautiana kuhusu tishio la kigaidi linaloikabili Amerika na maeneo mengine duniani.

Alipokua akijieleza mbele ya halmashauri ya vikosi vya Marekani, James Clapper, mkuu wa Idara ya ujasusi wa Marekani, alitangaza Alhamisi Februari 26 kwamba vitisho vya kigaidi dhidi ya Marekani na maeneo mengine duniani vimeongezeka.

“ Wakati tutakua tumekamilisha hesabu au uchunguzi kuhusu mashambulizi yaliotokea ulimwenguni, mwaka 2014 utakua ni mwaka uliokumbwa na maafa mengi tangu miaka 45 ilioorodheshwa”, amesema Clapper.

Clapper ameongeza kuwa katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka uliyopita, mashambulizi 13,000 yaligharimu maisha ya watu 31,000 duniani. Mengi miongoni mwa mashambulizi haya yalitekelezwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Taarifa hii ya mkuu wa Idara ya ujasusi wa Marekani inatofautiana na ile ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, aliyoitoa mbele ya Baraza la wawakilishi ndani ya massa 24 kabla.

“ Raia wa Marekani na ulimwenguni kwa ujumla wanaishi katika wakati ambapo vitisho vya kigaidi vya kila mara vimepungua ikilinganishwa na jinsi ilivyokuwa”, amesema John Kerry.

Kutofautiana huko kwa maneno, kumezua minong'ono na mvutano baina ya Wawakilishi wa raia na Idara za usalama.

Mkuu wa zamani wa Idara ya ujasusi ya Pentagone amemtuhumu Kerry kwamba alipewa taarifa zisio sahihi.

Upande wa chama cha Republican, wanabaini kwamba utawala wa Obama unajaribu kupuuzia vitisho vya kigaidi ili kuonyesha raia kuwa utawala huo unaendelea vizuri na mpango wake wa kupiga vita ugaidi unaotekelezwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.