Pata taarifa kuu
MARREKANI-AFGHANISTAN

Rais Obama akutana na viongozi wa Afghanistan jijini Washington

Rais wa Syria Bashar Al Assad amempokea kwa mazungumzo hii leo waziri wa mambo ya nje wa Iraq Ibrahim Al Jaafari ambae ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu ya Irak kuzuru nchini Syria tangu kuanza kwa machafuko mwaka 2011.

John Kerry waziri wa mambo ya nje wa Marekani na rais wa Afghanistan Ashraf Ghani
John Kerry waziri wa mambo ya nje wa Marekani na rais wa Afghanistan Ashraf Ghani REUTERS/Gary Cameron TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano na rais Assad, waziri wa Mambo ya nje wa Irak Ibrahim Al Jaafari na mwenyeji wake wa Syria Walid Mualem walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambapo, waziri Jaafari amesema amrkutana na rais Assad na kubaini kwamba ziara yake hiyo itazidisha kiwango cha ushirikiano kati ya Iraq na syria na katika kuabiliana na tishio lililopo kwa nchi hizi mbili rafiki.

Mwezi Juni mwaka 2014 serikali ya Damascus ilifahamisha kuwa tayari katika kushirikiana na Bagdad katika kukabiliana na hali ya hatari iliopo inayo sababishwa na kundi la Islamic State lililoyateka maeneo kadhaa ya nchi hizo mbili.

Upande wake waziri Mualem amesema kwamba nchi hizo mbili zipo katika harakati za kupambana na ugaidi na kwamba wanafanya kila jitihada kushirikiana katika vita hivi.

Hayo yanajiri wakati huu Marekani ikiendelea kuisaidia serikali ya Bagdad katika vita dhidi ya Islamic State kuurejesha kwenye himaya yake mji wa Tikrit kutoka mikononi mwa kundi hilo.

Muungano wa majeshi unaongozwa na Marekani umeendesha mashambulizi ya anga katika ngome za islamic State katika mji wa Tikrit na kutowa mafunzo na vifaa kwa wanajeshi wa Iraq, na hii ikiw ani mara ya kwanza inathibitishwa ushirika wa Marekani katika vita vya kuukomboa mji wa Tikrit uliochini ya himaya ya islamic State tangu mwaka 2014.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.