Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN-DIPLOMASIA-USALAMA

Barack Obama: “ wanajeshi wa Marekani watasalia Afghanistan”

Rais wa Marekani, Barack Obama amebadilisha uamuzi wake wa awali wa kuwaondoa wanajeshi wake wanaofikia elfu 5 nchini Afghanistani na badala yake sehemu kubwa ya wanajeshi hao wataendelea kusalia hadi mwakani.

Ashraf Ghani et Barack Obama wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Jumanne Machi 24, katika Ikulu ya White House.
Ashraf Ghani et Barack Obama wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Jumanne Machi 24, katika Ikulu ya White House. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amesema haya kufuatia ombi la rais wa Afghanistani, Ashraf Ghani ambaye aliomba wanajeshi wa Marekani waendelee kusalia nchini humo kusaidia kulinda usalama na kutoa ushauri kwa maofisa wa serekali waliochukua jukumu rasmi la kulinda usalama.

Rais Ghani amesema hatua hii ni faraja kwao kwa kuwa itasaidia kuelekea mabadiliko ya kiusalama wanayotarajia.

Katika hatua nyingine, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amesema nchi yao itaendelea kushirikiana na Afghanistani, ambapo ametoa wito kwa wapiganaji wa Taliban kutumia mwanya wa mazungumzo kufikia suluhu ya kudumu nchini humo.

Hivi sasa nchi ya Marekani ina zaidi ya wanajeshi elfu 9 na 800 walioko nchini Afghanistan.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.