Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-IS-USALAMA

Obama aungwa mkono kwa mradi wa amani wa nyuklia wa Iran

Rais wa Marekani Barack Obama amefanikiwa kupata uungwaji mkono kutoka kwa Maseneta kuwazuia wale wa Republican kupinga kupitisha mswada kuhusu mradi wa amani wa nyuklia wa Iran.

Mbele ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Washington, Barack Obama akielezea hoja yake ya kusaini mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Mbele ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Washington, Barack Obama akielezea hoja yake ya kusaini mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Jonathan Ernst

Matangazo ya kibiashara

Maseneta wa Democratic wameugana kumuunga mkono rais Obama, uamuzi ambao ni pigo kwa maseneta wa Repblican ambao wameweka wazi kupinga mktaba huo.

Kupitishwa kwa mktaba huo inamaanisha kuwa Marekani itaondoa vikwazo vya kuucumi dhidi Iran kama mojawapo ya makubaliano ya utekelezwaji wa mradi huo wa nyuklia.

Bunge la Congress linatarajiwa kujadili na kuupigia kura mkataba huo tarehe 17.

Hayo yakijiri vikosi maalum vya Marekani vinaendelesha mashambulizi ya angaa dhidi ya kundi la Islamic State kwa lengo la kumuua kiongozi wa kundi hilo nchini Syria.

Gazeti la Marekani la Washington Post limeandika kuwa hii ni operesheni maalum tofauti na ile inayowalenga wapiganaji na wa Islamic State.

Hadi sasa inaelezwa kuwa mashambulizi ya vikosi hivyo maalum yamesababisha kifo cha Junaid Hussain raia wa Uingereza mmoja wa Majihadi ambao wamekuwa wakisajili vijana kujiunga na kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.