Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Syria: mkutano wa kijeshi kati ya Urusi na Marekani

Urusi na Marekani wamekubaliana Jumatano wiki hii kwa mkutano wa dharura ili kuepuka tukio lolote la kijeshi kati ya operesheni zao nchini Syria baada ya mashambulizi ya kwanza ya Urusi ambayo yaliishangaza Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na Waziri mambo ya nje wa Marekani John Kerry mbele ya vyombo vya habari Septemba 30, 2015 kwenye makao Umoja wa Mataifa, mjini New York.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na Waziri mambo ya nje wa Marekani John Kerry mbele ya vyombo vya habari Septemba 30, 2015 kwenye makao Umoja wa Mataifa, mjini New York. DOMINICK REUTER/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliogubikwa na mgogoro wa Syria, siku mbili baada ya mkutano wa kilele mjini New York kati ya Barack Obama na Vladimir Putin, Urusi imetekeleza mashambulizi nchini Syria, na hivyo kuzua wasiwasi mkubwa kwa nchi za Magharibi kuhusu malengo ya Urusi: kuwaangamiza wapiganaji wa kundi la Islamic State au kuimarisha utawala wa rais wa Syria Bashar al-Assad?

Kwa mshangao mkubwa, Urusi iliendesha mashambulizi yake ya kwanza Jumatano wiki hii kwa ombi la rais wa Syria. Kremlin imesema ilikua inatakiwa kuwadhibiti "magaidi" kwa kasi na kuharibu ngome zao nchini Syria, kabla ya wao kuja kutekeleza mashambulizi mbalimbali " nchini mwetu ".

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, amekutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wawili hao wametangaza wakiwa pamoja mbele ya vyombo vya habari kwamba wamekubaliana juu ya haja ya mkutano " kati ya majeshi, utakaofanyika haraka iwezekanavyo, pengine hata kesho " ili " kuzuia tukio lolote " kati ya vikosi vya vyao vinavyoendesha mashambulizi ya anga nchini Syria.

Mkutano huu kati ya majeshi mawili yatazingatia kile John Kerry alichokiitwa kwa Kiingereza " deconfliction ". Hii inamaanisha kuepuka tukio la kijeshi kati ya ndege za Urusi na zile za muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, muungano ambao tangu mwaka jana umeendelea kushambulia ngome za kundi la Islamic State (IS).

Hayo yakijiri upinzani nchini Syria umesem akuwa mashambulizi ya Urusi nchini humo yamegharimu maisha ya watu wa kawaida 36.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.