Pata taarifa kuu
MAREKANI

Hillary Clinton na seneta Sanders watupiana maneno makali kwenye mdahalo wa ana kwa ana

Hillary Clinton usiku wa kuamkia leo amemshambulia kwa maneno mpinzani wake anayewania kwenda ikulu ya Marekani, Seneta Bernie Sanders, akimtuhumu kuendesha kampeni mbaya dhidi yake.

Seneta Bernie Sanders (Kushoto) akiwa na mgombea mwenzake Hillary Clinton wakati wa mjadala wa usiku wa kuamkia leoier 2016, à Durham dans le New Hampshire.
Seneta Bernie Sanders (Kushoto) akiwa na mgombea mwenzake Hillary Clinton wakati wa mjadala wa usiku wa kuamkia leoier 2016, à Durham dans le New Hampshire. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Katika mdahalo uliodumu kwa karibu saa mbili katika chuo kikuu cha New Hampshire mjini Durham, umefanyika ikiwa ni siku tano tu zimesalia kabla ya wananchi wa Hampshire kupiga kura za awali.

Mdahalo huu umefanyika ikiwa pia ni siku chache tu zimepita toka Hillary Clinton apate ushindi mwembamba kwenye mji wa Iowa.

Wakati huu watu wengi wakiamini kuwa Hillary Clinton atapitishwa na chama chake cha Democatic kuwania urais kwenye uchaguzi ujao, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa mpinzani wake wa karibu Bernie Sanders mwenye umri wa miaka 74 hivi sasa ambaye amepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa vijana.

Katika mdahalo wao wa kwanza kufanyika na kukutana wenyewe wawili tu, Hillary Clinton alitumia mdahalo huo kumkosoa mpinzani wake huku akijinasibu kuwa ni kinara wa mabadiliko na maendeleo atakayewasaidia raia wa Marekani iwapo atachaguliwa.

Hillary Clinton amesema kuwa yeye pamoja na Seneta Sanders wanakubaliana kwenye mambo mengi ya maendeleo, lakini haoni ni kwanini mpinzani wake ameanza kufanya kampeni mbaya dhidi yake.

Akijibu matamshi ya Clinton, seneta Sanders amesema kuwa mpinzani wake hawezi kudai kuwa yeye anamsimamo wa kati na pia mtu anayetaka maendeleo, akimkosoa kwa kuchangisha kiasi cha dola za Marekani milioni 15 toka kwenye soko la hisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.