Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Meli kubwa ya Marekani yawasili Cuba baada ya miaka 50

Cuba imekaribisha Jumatatu hii kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 meli ya kifahari ya Marekani, kutokana na kufufuliwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Washington na Havana, sawa na kuwasili kwa watalii wapya katika kisiwa hicho kinachoongozwa na utawala wa kikomunisti.

Wacuba wakiangali jinsi meli ya kwanza Marekani ikiwasili baada ya nusu karne katika bandari ya Havana, Mei 2, 2016.
Wacuba wakiangali jinsi meli ya kwanza Marekani ikiwasili baada ya nusu karne katika bandari ya Havana, Mei 2, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi kabla ya saa 4:30 mchana (sawa na saa 8:30 mchana saa za kimataifa), meli hii ijulikanayo kwa jina la Adonia ya shirika la Fathom, tawi la shirika la Marekani la Carnival, imewasili katika mji wa Havana, chini ya jua kali, huku maelfu ya raia wakimiminika katika bandari ya mji huo kuja kujionea kwa macho yao meli hiyo, huku bendera za nchi hizo mbili zikipeperushwa juu ya meli hiyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Raia wa Cuba wamepongeza kuwasili kwa meli hiyo ya Marekani, huku wakiiangalia jinsi inavyoegesha kwenye bandari.

"Kwangu mimi, ni ajabu, ninafuraha kubwa," ameliambia shirika la habari la AFP Yaney Cajigal, mwenye umri wa miaka 32, ambaye alikua amekuja kumpokea mpwa wake ambaye alikuwa amesafiri katika meli hiyo.

Abiria hawa waliosafiri na meli hii, "tunawapokea kwa bendera ya Cuba na ya Marekani ili kuonyesha kuwa tumekua na umoja, amani na utulivu," Cajigal ameongeza.

Meli ya kifahari ya Marekani iliondoka Miami Jumapili usiku na kutua katika moja ya bandari ya Cuba Jumatatu hii.

Meli hiyo imebeba abiria wapatao mia saba na bado inaendelea na safari yake na inatarajiwa kufika tamati ya safari yake Jumatatu ijayo.

Safari hiyo ya kihostoria kwa njia ya maji imepiga hatua moja kubwa mbele katika kuuimarisha uhusiano huo wa kidlomasia na hii ni baada ya serikari ya Cuba kukubali kuondoa marufuku ya raia wake kuingia nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.