PAKISTAN - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 03 februari 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 03 februari 2012

Wanajeshi 8 wa Pakistan wauawa katika shambulio la wanamgambo wa Taliban

Wapiganaji wa Taliban ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Pakistan
Taliban militants
Reuters/Mohammad Shoiab
Wapiganaji wa Taliban ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Pakistan

Na Emmanuel Richard Makundi

Wanajeshi saba wa jeshi la Pakistan wameripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya katika shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa kundi la Taliban jimboni Shidano Dand.

Wanamgambo wa Taliban walitekeleza shambulio hilo usiku wa kuamkia leo katika kituo cha ukaguzu kaskazini mwa nchi hizo kwenye mji wa Kurrama na kuwashambulia askari waliokuwa doria na kuwaua wanajeshi saba.

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Pakistan, amesema kuwa mbali na kupoteza wanajeshi saba lakini jeshi lake limefanikiwa kuwaua wanamgambo zaidi ya kumi na nane baada ya kutokea makabiliano ya risasi kati yao.

Eneo hilo ambalo ndilo ngome za wapiganaji wa Al-Qaeda na wanamgambo wa Taliban limekuwa kama ndio kitovu cha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali katika vituo vingi vya ukaguzi vinavyosimamiwa na wanajeshi wa Pakistan.

Shambulio hilo limekuja ikiwa zimepita siku mbili tu, toka wanamgambo hao wafanye shambulio la kushtukiza kwenye eneo hilohilo na kuua wanajeshi nane wa Pakistan.

tags: Pakistani
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close