CHINA -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatatu 20 agosti 2012 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumatatu 20 agosti 2012
Mke wa mwanasiasa maarufu nchini China ahukumiwa kifo
Gu Kailai akiwa mbelew ya mahakama
REUTERS/CCTVGu Kailai mke wa mwanasiasa maarufu nchini China Bo Xilai amehukumiwa kifo cha kumuua mfanyibiashara raia wa Uingereza Neil Heywood mwaka uliopita.
Wakati wa hukumu hiyo, Gu Kailai alisalia kimya huku akisomewa mashtaka ya kumuua mfanyibiashara huyo kwa kumpa sumu .
Hukumu aliyopata inaaminisha kuwa atasalia gerezani maisha yake yote,huku mshirika wake Zhang Xiaojun walioshirikiana kumuua mfanyibiashara huyo akihukumiwa kifungo cha miaka 9.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa Gu alikiri kumpa sumu mfanyibiashara huyo katika hoteli moja mjini Chongqing.
Aliongeza kuwa aliamua kuchukua uamauzi huo baada ya Heywood kumtisha mwanae wa kiume kuhusu makubaliano ya umiliki wa mali.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya