Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-UGAIDI-DOLA LA KIISLAM

Australia: operesheni kabambe dhidi ya ugaidi katika maeneo wanakoishi waislam

Mamia ya askari polisi wamemiminika alhamisi asubuhi wiki hii katika maeneo wanakoishi watu kutoka jamii ya waislam nchini Australia kwa lengo la kuwasaka watu wenye uhusiano na makundi ya kigaidi.

Askari polisi wakiwa mbele ya makaazi ya mmoja wa washukiwa waliokamatwa.
Askari polisi wakiwa mbele ya makaazi ya mmoja wa washukiwa waliokamatwa. REUTERS/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Watu 15 wamekamatwa katika operesheni hiyo, baadhi wameonekana kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Islamic State wanaoendeleza machafuko nchini Syria na Iraq.

Ni operesheni ya kwanza dhidi ya ugaidi kufanyika katika aridhi ya Australia. Askari polis 800 wameendesha msako katika maeneo 12 ya mji mkuu wa Australia, Sydney, na kuwakamata washukiwa 15. Omarjan Azari, raia wa Australia, mwenye umri wa miaka 22 ni miongoni mwa washukiwa hao.

Raia huyo wa Australia anadaiawa kuwa amekua akiwasiliana mara kadhaa na Mohammed Ali Baryalei, raia mwengine wa Australia nwenye asilia ya Afhanistan, ambaye anachukuliwa kama mmoja wa viongozi wa wapiganaji wa Dola la Kiislam (Islamic State), kwa mujibu wa waziri mkuu wa Australia Tony Abbott. Mafunzo yake yanahusu kuwaua raia wa Australia wanaokamatwa, na kurusha kwenye vyombo vya habari matukio hayo kama ilivyo kua hivi karibuni kwa mateka kutoka mataifa magharibi waliyochinjwa na wapiganaji hao nchini Syria.

Polisi imefaulu kuzima mashambulizi hayo. Kwa mujibu wa waziri wa uhamiaji wa Australia, Scott Morrison, hali hiyo inaonesha kuwa Australia inakabiliwa na tishio la kigadi . Juma liliyopita, serikali ilionesha jinsi gani kiwango cha tahadhari ya mashambulizi ya kigaidi kimepanda. Serikali ina hofu ya kuwepo kwa zaidi ya raia sitini wa Australia nchini Syria na Iraq waliojiunga na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kurejea kwa watu hao nchini Australia inaongeza hofu ya kushambuliwa kwa taifa hilo. Hata hivo wanajeshi 800 watatumwa alhamisi wiki hii nchini Saudia Arabia kujiunga katika kikosi cha Muungano wa kimataifa ambao unatazamiwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganji wa Dola la Kiislam. Wanajeshi 200 wa kikosi maalumu ni miongoni mwa wanajeshi hao ambao watatumwa nchini Saudia Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.