Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO

Hali yazidi kuwa mbaya jijini Hong Kong

Hali ya taharuki imezuka tena jijini Hong Kong wakati huu waandamanaji wanaodai mabadiliko ya kidemokrasia wakikabiliana na watu wanaopinga maandamano hayo ambao walikuwa wamejifunika uso.

Vijana wanaopiga
Vijana wanaopiga REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Vurugu zimeshuhudiwa mchana wa leo jijini Hong Kong baada ya kundi la watu waliojifunika uso ili wasitambulike, kujitokeza katika barabara kubwa waliokukusanyika waandamanaji na ambao wamepiga kambi sasa ni zaidi ya siku kumi na tano, na kuanza kuondowa vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji hao.

Polisi jijini Hapo ililazimika kuingilia kati ili kuepusha vurugu zaidi ambapo watu watatu wametiwa nguvuni kwa kosa la kuanzisha vurugu na kumiliki silaha.

Waandamanaji hao wanalituhumu jeshi la Polisi kuwasaidia watu hao wanaopinga maandamano kuwafikia eneo walipo kwa kuondowa vizuizi vilivyowekwa.

Vurugu kama hizo zilishuhudiwa siku kumo zilizopita katika mtaa wa kibiashara wa Mongkok ambapo watu 19 walitiwa nguvuni ambapo nane ni miongoni mwa wanaopinga maandamano.

Maandamano hayo yaliopelekea kuwekwa vizuizi tangu septemba 28, yanadhohofisha shughuli katika jiji la Hong Kong, na kuweka hatarini maisha ya watu zaidi ya milioni saba wa jiji hilo lililopo chini ya umiliki wa China na ambalo limeingia katika mzozo mkubwa kuhwahiu kushuhudiwa tangu mwaka 1997.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.