Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-Maandamano-Usalama-Siasa

Polisi yaanza kuwaondoa waandamanaji Hong Kong

Polisi Hong Kong wameanza kuwaondoa waandamanaji wa kisiasa katika kambi kuu ya kisiasa katika mji huo, eneo ambalo wamekuwa wakipiga kambi kwa miezi miwili sasa.

Erwiana Sulistyaningsih, mmoja wa wanasiasa wanataka kuwepo kwa mfumo wa kidemokrasia Hong Kong, akiwasili mahakamani Hong Kong, desemba 8 mwaka 2014.
Erwiana Sulistyaningsih, mmoja wa wanasiasa wanataka kuwepo kwa mfumo wa kidemokrasia Hong Kong, akiwasili mahakamani Hong Kong, desemba 8 mwaka 2014. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa Hong Kong ulikuwa umewaonya waandamanaji hao kuondoka katika kambi hiyo, wito ambao uliitikiwa na wengine na baadhi yao wakakataa kuondoka.

Idadi ya waandamanaji katika barabara za za Hong Kong imepungua kutoka maelfu hadi mamia kuanzia mwezi Septemba tangu walipoanza kuondolewa na polisi.

Polisi wamesema wamewapaa wandamani hao hadi Alhamisi Desemba 11 saa tatu asubuhi saa za Hong Kong kuondoka au la, watatumia nguvu kuwaondoa katika kambi hiyo.

Waandamanaji hao wa kisiasa wengi wao wakiwa wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wakishinikiza serikali ya China kuacha kuingilia maswala ya siasa katika eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2017.

Aidha, wanataka Beijing kutoingilia suala la uteuzi wa wagombea wa eneo hilo kama livyokuwa hapo awali, shinikizo zinazooneka kutoitikisa serikali ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.