Pata taarifa kuu
URUSI-PUTIN-UCHUMI

Putin : mdororo hautadumu zaidi ya miaka miwili

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameelezea Alhamisi Desemba 18 kupambana na mdororo wa uchumi wakati wa mkutano wake wa kila mwaka na vyombo vya habari, ambao unafikia tamati wakati ambapo fedha za Urusi zikiendelea kupoteza thamani.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wakati wa mkutano na vyombo vy habari Desemba 18 mwaka 2014.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wakati wa mkutano na vyombo vy habari Desemba 18 mwaka 2014. REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

Katika sekta ya uchumi, Putin ameonyesha baadhi ya matumaini akitoa ahadi ya miaka miwili kuwa fedha ya Urusi itakua imerejesha hadhi yake. amesema pia kuhusu machafuko yanayoendelea kila kukicha nchini Ukraine, vikwazo vinavyochukuliwa na mataifa ya magharib na kukemea kuundwa upya kwa "ukuta" barani Ulaya.

Katika ufunguzi wa mkutano wa kila mwaka na vyombo vya habari, kama kawaida yake, Vladimir Putin ameanza na suala la uchumi. Rais huyo wa Urusi alitaka kuanza na idadi chanya. ameelezea biashara ya nje au kiwango cha chini cha ukosefu wa ajira, ambacho kimefikia sasa kwenye asilimia.

Lakini amekubali mapema kuwa kupoteza thamani kwa fedha za Urusi kumeendelea kuwatia wasiwasi raia wa Urusi. Kwa njia ya moja kwa moja, Putin amekosoa hatua ya Benki kuu, ambayo haijachukua hatua muhimu kwa wakati. Putin amemtaja na kumuweka hatarini, Elvira Nabiouillina, Gavana wa Benki kuu, akisisitiza kuwa serikali ilihusika kwa sehemu moja, kwa sababu bila shaka, uchumi wa Urusi haukukusanya sekta zote.

Serikali imetakiwa kuchukua hatua mpya hususan kudhibiti bei za petroli na bei za chakula. Putin amesisitiza kuwa hazina ya fedha ya Urusi ya dola bilioni 419 inaiwezesha kutimiza ahadi zake za kijamii, ikiwa ni pamoja na malipo ya pensheni na mishahara. Lakini ametangaza kwamba bajeti itarejelewa upya, kupunguzwa kwa bajeti, huku akithibitisha kwamba ni lazima kuchukua angalau miaka miwili kabla ya kurejea ngazi ya ukuaji sahihi.

Kuhusu Ukraine, rais Putin hajabadili msimamo wake. Putin anazishutumu nchi za magharibi kujenga upya "ukuta" barani Ulaya ambao wanataka uchukuliwe kama "himaya" ambayo “ itanyemelea kwenye migongo ya waminifu wake."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.