Pata taarifa kuu
UFILIPINO-PAPA FRANCIS-JAMII

Papa Francis ufilipino: "Hatma ya Kanisa ni barani Asia"

Papa Francis amehitimisha ziara yake nchini Ufilipino Jumapili januari 18 kwa maadhimisho ya misa kubwa katika eneo la Rizal Park mjini Manila.

Papa katika akiongoza misa ya kukamilisha ziara yake nchini Ufilipino, ambapo waumini milioni 6 walihudhuria misa hiyo.
Papa katika akiongoza misa ya kukamilisha ziara yake nchini Ufilipino, ambapo waumini milioni 6 walihudhuria misa hiyo. REUTERS/Erik De Castro
Matangazo ya kibiashara

Waumini milioni sita walihudhuria misa hiyo, idadi ambayo imeonekana kuwa ya kwanza katika historia ya upapa.

Baada ya kushuhudia idadi hiyo ya waumini wa Kanisa Katoliki ambao walihudhuria misa ya kuhitimisha zaira yake, Papa Francis amebaini kwamba “ hatma ya Kanisa Katoliki ni barani Asia”.

Papa Francis ameifanya ziara yake ya kikazi nchini Ufilipino baada ya miezi mitano akiifanya ziara kama hiyo nchini Korea Kusini.

Nchini Sri Lanka, ambapo ilikua ni hatua ya kwanza ya ziara yake, Papa Francis alihubiria maridhiano kati ya watu kutoka jamii za Cinghal na Tamils, huku akitoa wito kwa mazungumzo kati ya dini mbalimbali. Katika ziara hiyo, Papa Francis alikumbuka kwamba uhuru wa dini ni haki ya msingi ya binadamu.

Nchini Ufilipino, Papa Francis aliunga mkono ushirikiano kati ya vijana na familia. alisema ni vema watu masiki watembele na wasaidiwe, huku akitia mkazo kwa kutembelea kitua kincholea watoto wa mitaani, ambao waliathiriwa na madawa ya kulevya na ukahaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.