Pata taarifa kuu
JAPANI-IS-MATEKA-USALAMA

Japani yakumbwa na kizungumkuti cha IS

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu inaloshikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria, limetishia katika mkanda wa video kuwaua raia wawili kutoka Japani ambao liinawashikilia mateka.

Tishio la kundi la Dola la kiislamu kimetolewa kwa mateka wa Japani wakati Wazirimkuu wa taifa hilo akiwa ziaranii Mashariki ya Kati. Jumanne Januari 20 asubuhi, Abe alikuwa Israeli kisha alisafiri amejielekeza Ramallah katika.
Tishio la kundi la Dola la kiislamu kimetolewa kwa mateka wa Japani wakati Wazirimkuu wa taifa hilo akiwa ziaranii Mashariki ya Kati. Jumanne Januari 20 asubuhi, Abe alikuwa Israeli kisha alisafiri amejielekeza Ramallah katika.
Matangazo ya kibiashara

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu linadai serikali ya Japani fidia ya dola milioni 200 kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu hao. Kundi hilo limetoa masaa 72 kwa serikali ya Japani ili iwe imeshalipa pesa hizo. Tokyo haikuchelewa kujibu, ikithibitisha kwamba haitashinikizwa wala kutishwa na ugaidi.

Akiwa ziarani Jerusalem, Waziri mkuu wa Japani, Shinzo Abe, amesema akisisitiza leo Jumanne Januari 20 kwamba serikali yake haitothubutu kutoa fidia hio iliombwa na mtu aliyevalia nguo nyeusi, huku akijifunika uso, akidai kwamba ni afisa wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, ambaye alionekana katika mkanda wa video akiwa na mateka hao wawili wa Japani ambao wamevaa mavazi ya rangi ya machungwa.

Katika ziara yake Mashariki ya Kati, Shinzo Abe amesema kusikitishwa mno na tukio hilo, na kuongeza kuwa hatositisha msaada usiyokuwa wa kijeshi wa dola milioni 200 aliyoahidi kwa mataifa yanayoendesha vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

Katika mkanda wa video, mtu aliyejificha uso ameiambia serikali ya Japan kuamua kuokoa maisha ya raia wake au kuendelea kuunga mkono mataifa ya nayowapiga vita.

" Dola milioni 200 ziliyoombwa kama fidia ili kuokoa maisha ya mateka zitasaidia kukabiliana na kiasi kama hicho, ambacho ni ahadi ya Japani kwa nchi zinazoendesha vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu", amesema mtu huyo katika mkanda wa video. Serikali ya Japan imepewa masaa 72 ili iweimesha lipa pesa hizo.

Mateka wa kwanza anaitwa Kenji Goto. Ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ambaye amekua akizitumia televisheni za Japan picha za maeneo ya vita katika nchi za Mashariki ya Kati. Mateka mwingine anaitwa Harumi Yukawa. Mmiliki wa kampuni ndogo inayojishughulisha na masuala ya usalama katika mji wa Tokyo, ambayo ilifilisika. Alikuwa amesusiwa na vyombo vya habari vya Japani baada ya kutekwa nyara nchini Syria mwezi Agosti mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.