Pata taarifa kuu
YEMEN-Mapigano-Siasa-Usalama

Waziri mkuu wa Yemen aomba kuondoka katika makazi yake

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Yemen, Waziri mkuu Khaled Bahah ameondoka katika makazi yake mjini kati Sanaa, ambapo alikua chini ya ulinzi mkali wa wanamgambo wa Kishia tangu Jumatatu Januari 19 mwaka 2015, baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya kuodoka kwake katika makazi hayo.

Wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Houthi karibu na ikulu ya rais katika mji wa Sanaa, Januari 21 mwaka 2015.
Wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Houthi karibu na ikulu ya rais katika mji wa Sanaa, Januari 21 mwaka 2015. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu ameondoka katika makazi hayo na kupelekwa “eneo lenye usalama”.

Jumatatu Januari 19 jioni, wanamgambo wa Kishia wakiwa na silaha za kivita walizingira makazi ya Waziri mkuu, Khaled Bahah, saa chache baada ya msafara wake kushambuliwa.

Msafara wa Waziri mkuu huyo ulishambuliwa na wanamgambo wa Kishia baada ya kushiriki katika mkutano uliyoitishwa na rais Abd Rabbo Mansour hadi. Kwa mujibu wa Waziri wa habari, Nadia al-Sakkaf, Khaled Bahah hakujeruhiwa katika mashambulizi hayo dhidi ya msafara wake.

Mapiganao makali yaliripotiwa Jumatatu na Jumanne kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa Kishia katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Yemen, Sanaa, na kusababisha vifo vya watu 35 na makumi ya watu kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya hospitali. Wanamgambo hatimaye walichukua udhibiti wa Ikulu ya rais kusini mwa mji wa Sanaa tangu Jumanne Januari 20.

Wanamgambo wakana kumtimua rais madarakani

Mapema Jumatatu wiki hii, rais wa Yemen, Abd Rabbo Mansour Hadi, amempokea katika boma lake mjini Sanaa mmoja kati ya washauri wake anaewakilisha wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Houthi, kwa mujibu wa watu walio karibu na rais. Mbali na mshauri huyo, Saleh al-Sammad, rais wa Yemen amewapokea kwa mazungumzo wawikilishi na wakuu wa wakoo mbalimbali, ambapo amewafahamisha kwamba anaendelea na majukumu ya urais.

Wanamgambo wa Kishia wamekataa rasimu ya katiba kuhusu kugawanywa kwa shirikisho la nchi, huku wakidai kushirikishwa katika taasisi zote za uongozi wa nchi. Hata kama walichukua udhibiti wa makazi ya rais, wanamgambo hao wamekataa kuwa wamemtimua rais madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.