Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MATEKA-USALAMA-HAKI ZA BINADAMU

IS yawashikilia mateka mamia ya watu Syria

Wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu wameendesha mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa kaskazini mashariki mwa Syria, na kuwateka nyara mamia ya watu, zaidi ya 30 kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Raia kutoka jamii ya Wakristo waliokimbilia Libanon kutokana na mapigano kaskazini mashariki mwa Syria, Februari 26 mwaka 2015.
Raia kutoka jamii ya Wakristo waliokimbilia Libanon kutokana na mapigano kaskazini mashariki mwa Syria, Februari 26 mwaka 2015. AFP PHOTO / ANWAR AMRO
Matangazo ya kibiashara

Mamia kwa maelfu ya wakazi wa vijiji hivyo wamekimbilia katika miji mikuu ya mkoa, kama Hassaké au Qamichli.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mij wa Istanbul, Jérôme Bastion, mapigano yamekua yakiendelea usiku wa Alhamisi Februari 26, kando ya mto Khabour ambako kunapatikana vijiji hivyo ambavyo vinakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kislamu tangu Jumatau asubuhi wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa za mwisho tulizopokea kwa simu kutoka eneo hilo, hadi watu 350 wametekwa nyara katika vijiji hivyo. Inasadikiwa kuwa watu 110 miongoni mwa wanavijiji huenda waliuawa.

Kwa kweli inaaminika kuwa wanamgambo hao wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu waliwabeba wanawake na watoto katika mlima wa Abd al-Aziz, ulio karibu, ambao wameutenga kama ngome yao kuu.

Hata hivyo, wanamgambo hao wamewaacha vijijini wazee na wanaume kuwa kama ngao dhidi ya majeshi ya Kikurdi, na wapiganaji wa makundi mengine ambao wamekua wakijianda kujibu mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.