Korea Kusini : waziri wa Ulinzi anyongwa
Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un alimuua kwa risai waziri wake wa ulinzi kwa ajili ya uhaini na kutomuheshimu, imesema leo Jumatano asubuhi Idara ya ujasusi ya Korea Kusini. Waziri huyo wa ulinzi amliuawa hadharani kwa silaha nzito.
Imechapishwa:
Tangu kifo cha baba yake Kim Jong-il na kuingia kwake madarakani mwaka 2011, Kiongozi huyo kijana wa Pyongyang amekua akiwakunyonga baadhi ya washirika wake vigogo.
Visa vya kunyongwa kwa washirika vigogo wa kiongozi wa Korea Kaskazini vimeendelea kushuhudiwa tangu kiongozi huyo alipochukua madaraka baada ya kifo cha babake.
Kwa mujibu wa maafisa wa Upelelezi nchini Korea Kusini, waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, Hyon Yong-Chol, aliuawa mwishoni mwa mwezi Aprili mbele ya mamia ya viongozi vigogo wa Korea Kaskazini kwa kutumia bunduki inayodungua ndege ya kivita.
Waziri huo wa ulinzi aliteuliwa kwenye wadhifa huo mwaka mmoja uliyopita, na alituhumiwa na Kim Jong-un wa kukaidi amri zake katika maadhimisho ya kijeshi, na kutofuata maelekezo ya yake.