Pata taarifa kuu
INDIA-SHERIA-HAKI

India: mtuhumiwa wa mashambulizi ya Mumbai anyongwa

India imemnyonga Yakub Memon aliyepatikana na kosa la kufadhili mashambulizi ya kigaidi mjini Mumbai mwaka 1993.

Moja mashambulizi ya kigaidi yaliotokea katika jimbo la Mumbai, India.
Moja mashambulizi ya kigaidi yaliotokea katika jimbo la Mumbai, India. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya jimbo la Mahara shtra imethibitisha kumyonga Memon ambaye amekuwa akizuiliwa katika gereza la Nagpur katika jimbo hilo.

Mahakama ilimpata na hatia ya kufadhili shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 257.

Alipoulizwa ni kwanini alifadhili mashambulizi hayo alisema alifanya hivyo ili kulipiza kisasi baada ya serikali kuwavamia na kuwauwa waandamanaji wa Kislamu mwaka huo wa 1993.

Adhabu hii inakuja huku Mawakili wa Memon wakilaani hatua hiyo kwa kile wanachosema kuwa adhabu hiyo ingetekelezwa siku saba baada ya Mahakama ya rufaa kukataa shauri la msamaha.

Juhudi za wanaharakati wa haki za binadamu kumtetea Yakub Memon asamehewe ziliambulia patupu.

Hii ndio adhabu ya kwanza kutekelezwa nchini India tangu mwaka 2004.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.