Pata taarifa kuu
GUATEMALA-RUSHWA-UCHUMI-SIASA-SHERIA

Guatemala: wabunge wapiga kura ya kufuta kinga ya Otto Pérez

Nchini Guatemala, Bunge limepitisha bila kupingwa uamzi wa kufuta kinga ya Rais Otto Pérez. Uamuzi huu umefungua milango kwa kesi dhidi ya Rais wa nchi hiyo anayetuhumiwa kuongoza mtandao wa rushwa katika Idara ya forodha.

Raia wa Guatemala wakiandamana kwa furaha baada ya wabunge kupitisha uamzi wa kumuondolea kinga Rais Otto Pérez.
Raia wa Guatemala wakiandamana kwa furaha baada ya wabunge kupitisha uamzi wa kumuondolea kinga Rais Otto Pérez. REUTERS/Josue Decavele
Matangazo ya kibiashara

Rais Otto Pérez amegonga ukuta na sasa anaweza kufikishwa kizimbani. Baada ya kupoteza kinga yake, anaweza sasa kuhukumiwa kama raia yeyote. Na hata kama Otto Pérez atakataa kujiuzulu, afisa wa mashtaka anaweza kumwita kufika mbele ya jaji, jaji ambaye kwa upande wake anaweza kulazimisha Otto Pérez kuwekwa kizuizini. Kwa masharti, bila shaka ya kupatikana ushahidi na vielelezo vitakavyoonyesha iwapo anahusika na kashfa hiyo.

Hata hivyo Otto Pérez Jumamosi aliwasilisha rufaa kwa Mahakama ya Katiba dhidi ya ripoti ya kamati ya uchunguzi ya Bunge, kufuatia uamzi wa Bunge kumfutia kinga yake. Kama mahakama itapokea rufaa hiyo, tuhuma dhidi ya Rais zitasitisha kwa muda.

Mbali na Bunge, raia wa Guatemala, ambao kwa miezi kadhaa waliingia mitaani kulaani viongozi wa serikali wanaojihusisha na rushwa na kumtaka rais kujiuzulu, wamesheherekea uamuzi wa wabunge. Uamuzi, ambao siku chache tu kabla ya uchaguzi wa Jumapili, utapelekea hali ya taharuki inayoshuhudiwa nchini humo kupungua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.