Pata taarifa kuu
CHINA-ULINZI-USALAMA

Xi Jinping: China imekua tena "nchi kubwa duniani"

Ndege mia mbili zimeruka juu ya anga ya Beijing le Alhamisi, Septemba 3 asubuhi. Kumekua na gwaride la kijeshi, katika eneo la Tianamnen kwa kuadhimisha miaka 70 ya kujisalimisha kwa Japan na mwisho wa Vita kuu vya II vya dunia barani Asia.

Jeshi la watu wa Ukombozi limefanya gwaride katika mji wa Beijing kwa kuadhimisha mwisho wa Vita kuu vya pili vya dunia, miaka 70 baada ya kushindwa kwa Japan, Septemba 3, 2015 kweny barabara ya Tiananmen.
Jeshi la watu wa Ukombozi limefanya gwaride katika mji wa Beijing kwa kuadhimisha mwisho wa Vita kuu vya pili vya dunia, miaka 70 baada ya kushindwa kwa Japan, Septemba 3, 2015 kweny barabara ya Tiananmen. REUTERS/Xinhua/Pang Xinglei
Matangazo ya kibiashara

Vita hivyo viliwauawa zaidi ya milioni 15 ya raia wa China. Lakini siku hizi, Beijing imekua ikijisifu kama taifa lililokua zaidi katika sekta mbalimbali. Hayo aliyazungumza Rais Xi Jinping katika hotuba yake.

Kama watawala, ambao walipata uhalali wao kutoka mbinguni, Rais akiwa pia Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Watu wa China ameweza kusalimia askari wake, huku akisimama katika gari lake leusi, aina ya a limousine, katika jua kali kwenye barabara iliyopewa jina la Amani ya Mbinguni (Tianamnen).

Kutoka juu ya mlango wa kusini kwa mji, ambapo Mao alitangaza kuzaliwa kwa taifa la watu wa China tarehe 1 Oktoba mwaka 1949, Xi Jinping amewahutubia askari 12,000 ambao walikua wakimuangalia na kumfuata kwa makini anavyozungumza. "Mumefanya kazi kubwa ", amesema Xi. "Kwa kuwahudumia wananchi! ", askari walijibiu.

Askari wa China walivaa sare mpya za jeshi, na kuongeza bidhaa mbalimbali za China, amesema mwandishi wetu mjini Beijing, Heike Schmidt. Zaidi ya 80% vifaru, makombora, ndege za kivita za kisasa, magari 500 kwa jumla, pia yalionekana katika umma kwa mara ya kwanza. Kati vifaa hivyo, maelfu ya makombora mapya ya jeshi la China, DF-21D. Silaha hizi, ambazo zinaweza bado kupima takriban upeo, zinaongeza kwa miaka kadhaa katika mjadala katika maeneo ya kijeshi juu ya uwezo wao wa kubadilisha uwezo wa nguvu katika Bahari ya Pasifiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.