Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI NA KASKAZINI-MZOZO

Korea Kaskazini yawafukuza wafanyakazi wa Korea Kusini katika kiwanda cha pamoja cha Kaesong

Serikali ya Pyongyang imeamuru kuondoka mara moja kwa  wanfanyakaziwa Korera Kusini katika kiwanda cha pamoja cha Kaesong na kuhodhi mali zao baada ya hatuwa ya serikali ya Seoul kusitisha shughuli kufuatia mpango wake wa majaribio ya makombora.

wafanyakazi wa kiwanda cha pamoja cha Kaesong
wafanyakazi wa kiwanda cha pamoja cha Kaesong Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Hatuwa hiyo ya kuwafukuza wafanyakazi wa kiwanda hicho cha Kaesong kutoka Korea Kusini imekuja baada ya Jaribio la nne la makombora yaliofanywa na Korea kaskazini februari 6,.

kiwanda hicho kinachukuliwa kama ishara ya maridhiano baina ya Korea hizo mbili na sasa mzozo huo huenda ukazua mtafaruku mwingine ambao utadumu kwa kipindi kirefu.

Katika taarifa , ya kamati ya ya pamoja na muungano wa Korea hizo mbili na kuchapishwa na shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini KCNA, imefahamisha kwamba kiwanda cha kaesong imewekwa katika eneo linalo milikiwa pande zote mbili licha ya kwamba kipo katika eneo la Korea kaskazini chini ya ulinzii wa jeshi.

Mbali na kuwaondowa wafanyakazi katika kiwanda hicho njia mbili za mawasiliano ya simu kuelekea Seoul zimekatwa.

Ili kupinga uvunjifu wa sheria za maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa Nyuklia, serikali ya Seoul ilitangaza jana kusitisha shughuli zake katika kinwada cha pamoja kilicjopo kwenye umbali wa kilometa 10 na mpaka wake.

Serikali ya Pyongyang inasema kuchukuwa hatuwa hiyo ni kama vile kutangaza vita ambavyo vinaweza kuwa hatari sana.

Uhusiano kati ya pande hizo mbili umekuwa ukidorora mara kadhaa lakini sasa hivi wataalamu wanahofia kwamba huenda mzozo huo ukawa mkubwa zaidi ya ilivyo siku zote.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.