Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SENEGAL-Soka Barani Afrika-Can 2015

Afrika Kusini na Senegal zatoka sare ya bao 1-1

Afrika Kusini na Senegal zimetoka sare ya kufungana bao1-1, katika mchuano uliozikutanisha Ijumaa, Januari 23 mwaka 2015.

Mchezaji wa Afrika Kusini, Dean Furman (kushoto) akikabiliana na mchezaji wa Senegal Pape Kouli Diopi.
Mchezaji wa Afrika Kusini, Dean Furman (kushoto) akikabiliana na mchezaji wa Senegal Pape Kouli Diopi. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Senegal inaongoza katika kundi C ikiwa na alama nne, huku Bafana Bafana ikitiliwa mashaka ya kufuzu katika robo fainali ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika.

Afrika Kusini kama Ghana dhidi ya Algeria, haikua inapewa bahati ya kwenda sare na Senegal. Senegal haikushiriki michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kocha wa Bafana Bafana, Ephraim Mashaba, amesema timu ya taifa ya Afrika Kusini si mchezo kama wanavyofikiria wengi.

“ Tutacheza dhdi ya timu kubwa, timu ambayo ina mchezo mzuri ikilinganishwa na Ghana pamoja na Algeria, lakini ina upungufu kidogo kwenye safa ya ulinzi”, ameonya kocha wa Senegal Alain Giresse, kabla ya mchezo kati ya Senegal na Afrka Kusini kuanza.

Hata hivyo, Senegal ingeleweza kufunga katika dakika 45 kwa mpira wa kichwa uliopigwa na Mame Biram Diouf, lakini kwa bahati mbaya mpira uligonga kwenye mwamba na ukatoka nje. Hio ilikua bahati ya kwanza ya Senegal katika kipindi cha kwanza.

Baada ya kukataliwa kwa bao lililofungwa na Sadio mane kwa kosa la kuotea katika dakika 57, Serigne Kara M'Bodji alifaulu kuingiza bao la kusawazisha katika dakika 60.

Kundi C

Naf Timu M Al
1 Senegal 2 4
2 Ghana 2 3
3 Algeria 2 3
4 Afrika Kusini 2 1

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.