SYRIA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 17 machi 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 17 machi 2012

Kofi Annan atoa wito kwa umoja wa mataifa kuungana kukomesha machafuko nchini Syria.

Kofi Annan se dit prêt à retourner en Syrie pour poursuivre les négociations.
Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan
REUTERS/Denis Balibouse
Kofi Annan se dit prêt à retourner en Syrie pour poursuivre les négociations.

Na Martha Saranga Amini

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan pamoja na wajumbe wa mataifa ya kiarabu katika umoja wa mataifa kuhusu Syria wametoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuungana ili kusaidia juhudi za upatanishi dhidi ya mgogoro wa Syria.

Wito huo wa Annan kwa wajumbe wa baraza hilo kutoka mataifa 15 jana Ijumaa umekuja kufuatia maandamano ya kuipinga serikali kuendelea nchini Syria kutaka majeshi ya kimataifa kuingilia kati mgogoro huo.

Wanaharakati wamesema kuwa jumla ya watu 15 wakiwemo watoto wameuwawa katika vurugu hapo jana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Aidha wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema kuwa itashirikiana vema na Kofi Annan katika juhudiza kumaliza mgogoro wakati huohuo itapambana kupinga ugaidi.
 

tags: Kofi Annan - Syria - Umoja wa Falme za Kiarabu - Umoja wa Mataifa UN
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close