Syria - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatano 21 machi 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 21 machi 2012

Koffi Annan kurejea Damascus hivi karibuni wakati mapigano yakiendelea

mapigano yanaendelea nchini Syria
mapigano yanaendelea nchini Syria

Wapiganaji wa upinzani nchini Syria wanaendelea kupambana na wanajeshi wa serikali mjini Damascus na miji mingine wakati Urusi ikisema serikali ya rais Bashar Al Asaad inafanya makosa mengi katika harakati za kumaliza machafuko hayo.Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anasema mjumbe maalum wa umoja huo kuhusu mzozo wa Syria Koffi Annan anatarajiwa kurudi Damascus hivi karibuni kufanya mazungumzo zaidi na rais Bashar Al Asaad na viongozi wa upinzani.

Moon ametangaza hayo siku moja baada ya wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuafikiana kufanyia mabadiliko azimio dhidi ya rais Bashar Al Asaad baada ya Urusi kuendelea  kuwa kikwazo dhidi ya hatua kuchukuliwa dhidi ya rais Assad.

Mapendekezo ya hivi karibuni yanalenga kuonesha uungwaji mkono wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  kwa mjumbe wa UN Koffi Annan katika harakati zake za kutatua machafuko hayo ambayo yamesababisha kuuwa kwa zaidi ya watu elfu nane kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.

Mazungumzo ya Annan na viongozi wa upinzani yanalenga kusitisha mapigano yanayoendelea kwa sasa kabla ya kuanza mazungumzo ya kuleta maridhiano ya kisiasa nchini humo na pia kuwasaidia waathiriwa wa mapigano hayo kwa misaada ya kibinadamu.

Annan amekuwa akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzungumza kwa sauti moja dhidi ya mapigano nchini Syria na kuunga mkono juhudi zake za kupata suluhu.

Tayari msuluhishi huyo amekutana na rais Bashar Al Asaad na viongozi wa upinzani mapema mwezi huu na kutoa mapendekezo anayosema yatasaidia kumaliza mzozo huo.
 

tags: Ban Ki-moon - Bashar Al Assad - Syria - Umoja wa Mataifa UN - Urusi
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close