DR CONGO - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 19 mei 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 19 mei 2012

Majeshi ya Congo DR yashambulia kambi ya waasi Kivu

Wanajeshi wa jeshi la Congo DR
saidmihala.blogspot.com

Na Martha Saranga Amini

Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo limeshambulia ngome za makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo katika eneo la milima ya mbuzi na Tchanzu iliyoko kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Taarifa kutoka kwa jeshi hilo zinaeleza kuwa wapiganaji hao wanaomtii jenerali Jean Bosco Ntaghanda anayetafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC,wameweka ngome zao katika vijiji vya mpakani mwa Rwanda,Uganda na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Bosco Ntaghanda anatumia askari walioasi katika jeshi la nchi hiyo na kuendelea kufanya vitendo vinavyovunja haki za binadamu,ikiwemo mauaji na ubakaji.
 

tags: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close