SUDANI - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumapili 20 mei 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumapili 20 mei 2012

Rais Omar Al Bashiri akiri haja ya kuwepo na amani baina ya Sudani na Sudani Kusini.

Rais wa Sudani Omar al Bashir
zesham.blogspot.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Rais wa Sudan Omar Al Bashiri amesema kuwa ipo haja ya kuwa na amani kati ya Sudani na Sudani Kusini na kwamba Sudani inadhamira ya dhati katika mikataba ya amani ambayo imesaini.

Akinukuu kauli ya rais Bashir, mpatanishi wa Umoja wa Afrika Thabo Mbeki muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na rais Bashir, amesema kuwa rais Bashir amekiri kuwepo haja ya amani baina ya mataifa hayo mawili.

Mkutano huo umekamilisha siku mbili za mazungumzo na maafisa wa Sudan huku Mbeki akijaribu kuzishinikiza Sudan na Sudan Kusini kurejea katika mazungumzo ambayo yalisitishwa baada ya kutokea mapigano katika mpaka mwezi uliopita.

 

tags: Sudani Kaskazini - Sudani Kusini - Thabo Mbeki - Umoja wa Afrika AU
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close