MALAWI - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 09 juni 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 09 juni 2012

Malawi yajivua wenyeji wa mkutano wa Umoja wa Afrika AU

Rais wa Malawi Joyce Banda ambaye ametangaza nchi yake kujivua wenyeji wa mkutano wa AU
Rais wa Malawi Joyce Banda ambaye ametangaza nchi yake kujivua wenyeji wa mkutano wa AU
Reuters

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Malawi imetangaza kuahirisha kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilelel wa umoja wa Afrika uliopangwa kufanyika mwezi ujao nchini humo,kufuatia mzozo baina yake na umoja wa Afrika ambao unasisitiza kumualika rais wa Sudani Omar Al Bashir ambaye anatakiwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ICC.

Makamu wa Rais Khumbo Kachali amesema kuwa serikali imekataa kuwapigia magoti wanachama 54 wa Umoja wa Afrika kuhusu rais Bashir, ambaye anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita,kuhudhuria mkutano wa Lilongwe.

Mapema siku ya Alhamisi, Sudan ilitoa wito kwa umoja wa Afrika AU kuhamisha mkutano huo kutoka Liongwe Malawi na ufanyikie kwenye makao makuu yake mjini Addis Ababa Ethiopia baada ya Malawi kutangaza kuwa rais Bashir hakaribishwi nchini humo.

 

tags: Malawi - Omar Al Bashir - Sudani - Umoja wa Afrika AU
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close