Marekani yasema haikushangazwa na mabadiliko ya kijeshi nchini Misri

Marekani inasema ilitarajiwa kuwa rais wa Misri Mohammed Morsi anagefanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa kijeshi nchini humo.
Idara ya jeshi nchini Marekani ya Pentagon ambayo imekuwa ikishirikiana na jeshi la Misri kwa muda mrefu imesema itaendelea kushirikiana na jeshi la Misri katika maswala ya kijeshi kati ya mataifa hayo mawili.
Aidha, Washingtobn DC inatoa wito kwa serikali na jeshi kushirikiana ili kuimarisha maisha ya wananchi wa taifa hilo baada ya mapinduzi ya uongozi nchini humo mwaka uliopita.
Siku ya Jumatatu rais wa Misri Mohammed Morsi alitetea uamuzi wake wa kumwachisha kazi Waziri wa Ulinzi Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi, kwa kile alichokisema kuwa mabadiliko hayo ameyafanya kwa maslahi ya watu wa Misri
Rais Morsi anawataka wananchi wote wa Misri kumuunga mkono katika juhudi zake za kubadilisha uongozi wa taasisi mbalimbali nchini humo, jambo ambalo wachambuzi wa siasa za Misri wanaona kuwa mabadiliko aliyoyayaahidi rais Morsi yameanza kutekelezwa.
Aidha, Mosri amesema kuwa lengo lake halikuwa la kuwaibisha maafisa aliyowaachisha kazi wala taasisi ya kijeshi kwa kile alichokifafanunua kuwa mabadiliko hayo yalikuwa ni kwa manufaa ya wananchi wa Misri.
Kuondolewa kwa Tantawi kazini kunamaanisha kuwa baraza la kijeshi lililokuwa linaongoza nchi huyo baada ya mapinduzi ya mwaka uliopita limevunjwa.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya