DR Congo - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 18 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 18 agosti 2012

Jeshi la kimataifa la kupambana na makundi ya uasi Mashariki mwa Congo kuwa na askari 4,000

Waziri wa ulinzi wa DRC Alexandre Luba Ntambo
Waziri wa ulinzi wa DRC Alexandre Luba Ntambo
lecongolais.cd

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Jeshi la kimataifa linalobuniwa kwa lengo la kusaidia kurejesha amani mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,linatarajiwa kuwa na askari 4,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Waziri wa Ulinzi Alexandre Luba Ntambo amesema jana Ijumaa.

 

Jeshi hilo la kimataifa lisilofungamana na upande wowote halitajumuisha askari kutoka DR Congo wala nchi yoyote katika zile zinazotuhumiwa kuhusika katika mapigano katika jimbo la Kivu amesema waziri Ntambo, siku sita baada ya kukutana na mawaziri wengine wa ulinzi kutoka katika ukanda huo wa maziwa makuu, kukabiliana na machafuko.

Nchi ambazo hadi sasa zinatajwa kuhusika katika mapigano Mashariki mwa Congo ni pamoja na DRC, Rwanda, Burundi na Uganda, hivyo kujumuishwa kwazo katika jeshi hilo si sahihi amesema waziri Ntambo.
 

tags: Burundi - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - Rwanda - Uganda
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close