ANGOLA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 31 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 31 agosti 2012

Wananchi wa Angola wanapiga kura leo kumchagua rais wa nchi hiyo.

Raia wa Angola wakijiandaa kupiga kura
Raia wa Angola wakijiandaa kupiga kura
lexpress.fr

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Wananchi wa Angola wanapiga kura hii leo katika uchaguzi mkuu kumchagua rais wa nchi hiyo.

 

Rais Dos Santos ambaye anagombea kwa tiketi ya MPLA atapambana na mmoja wa wapizani wake wakuu Bwana Isaias Samakuva, ambaye ni kiongozi wa UNITA, chama ambacho zamani kimeendesha uasi kwa mda mrefu nchini humo chini ya uongozi wa Jonas Savimbi.

Uchaguzi huu unakuja miaka kumi baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo,na unafanyika katika kipindi ambacho kuna ongezeko la matatizo ya kijamii na ukomavu zaidi wa vyama vya upinzani.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uchaguzi huu utakuwa na changamoto ya aina yake kutokana na ukomavu wa vyama vya upinzani.

tags: Angola
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close