UGANDA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumapili 09 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumapili 09 septemba 2012

Mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu (ICGLR) wamalizika bila ufumbuzi wa amani Mashariki mwa DRC

Baadhi ya viongozi wa nchi za maziwa makuu wakiwa Kampala Uganda
presstv.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu kuhusu hali ya usalama mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umemalizika hapo jana jijini Kampala nchini Uganda huku kukiwa hakuna ufumbuzi wa kudumu katika machafuko sugu mashariki mwa nchi hiyo.

 

Viongozi chini ya theluthi moja walioalikwa wamehudhuria mkutano huo jijini Kampala,chini ya mwenyeji rais Yoweri Museven, jambo linaloashiria kuwa suala la kuundwa kwa jeshi huru lisilofungamana na upande wowote kutatua mzozo huo wa Congo bado litaendelea kuwa kitendawili.

Katika taarifa kufuatia mkutano wa Jumamosi, viongozi hao wa maziwa makuu wamesema kuwa iwapo jeshi hilo litaundwa litapelekwa nchini DRC kwa mamlaka ya Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa.

Viongozi hao pia wametoa wito kwa mawaziri wa ulinzi wa ukanda huo kuharakisha utendaji kuelekea kuanza kazi kwa jeshi huru la kimataifa ndani ya miezi mitatu.

tags: DRC - ICGLR - Rwanda - Tanzania - Uganda
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close