LIBYA - MAREKANI - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatano 12 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 12 septemba 2012

Marekani yalaani kitendo cha kushambuliwa na kifo cha balozi wake jijini Benghazi nchini Libya

Ubalozi mdogo wa Marekani jijini Benghazi ukiteketea kwa moto jana Septemba 11, 2012.
Ubalozi mdogo wa Marekani jijini Benghazi ukiteketea kwa moto jana Septemba 11, 2012.

Na Ali Bilali

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amelaani kitendo cha shambulizi lililotekelezwa nchini Libya katika Jiji la Benghazi na kusababisha kifo cha afisa balozi na mwengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia ubalozi wao.

Waandamanaji wenye hasira waliuvamia ubalozi wa Marekani jijini Benghazi sambamba na jijini Kairo kufuatia filamu ilioandaliwa na raia mmoja wa Marekani mwenye asili ya Israeli kuandaa filamu ilioonyesha wakati wa kumbukumbu za mashambulizi ya septemba 11 jijini New York.

waandamanaji hao walivamia ubalozi wa Marekani jijini Benghazi na kuteketeza kwa moto, baada ya kuonyeshwa filamu hiyo ilioudhalilisha uislam.

Serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje Hillary Clinton amekiri kusikitishwa na kukatishwa tamaa na kitendo hicho ambacho kinaelezwa kwenda sambamba na ghasia katika Ubalozi wa Marekani nchini Misri ambao nao walikuwa wanapinga kitendo cha kuoneshwa kwa filamu inayomdhihaki Mtume Muhammad na kuwadhalilisha waislam.

Waziri Clinton amesema kuoneshwa kwa filamu hiyo hakukuwa na uhusiano na kutekelezwa kwa mashambulizi kwenye Ubalozi wa Marekani na mapema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland alielezea ghasia za huko Misri.

tags: Hillary Clinton - Libya - Marekani - Misri
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close