Pata taarifa kuu
Somalia

Rais mpya wa Somalia anusurika kifo jijini Mogadishu

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud amepata msukosuko wa kwanza tangu ashinde uchaguzi siku ya jumatatu baada ya kushuhudia shambulizi la kujitoa mhanga likitekelezwa katika hotela ambayo alikuwa anakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Sam Ongeri.

Rais mpya wa Somalia Hassan Cheikh Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Cheikh Mohamud
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo la kwanza limetekelezwa wakati Rais Shaikh Mahmoud alipokuwa anakutana na Waziri Ongeri ambaye alikuwa ametumwa kupeleka ujumbe maalum kwa kiongozi huyokutoka serikali ya Kenya.

Picha za video ambazo zimeonesha tukio hilo zimemuonesha Rais Sheikh Mahmoud akimtuliza Waziri Ongeri wakati mlipuko na milio ya risasi ilipokuwa inaendelea nje ya Hotel hiyo na kumueleza asiwe na shaka kwa kuwa yupo kwenye mikono salama.

Askari watu wameuawa akiwemo mmoja wa Uganda na wengine wawili wa Somalia katika tukio hilo lililotekelezwa na washambuliaji watatu wa kujitowa mhanga

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.