Mali -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 15 septemba 2012 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 15 septemba 2012
Wanaume watano nchini Mali wakatwa viungo kwa tuhuma za wizi, ikiwa ni utekelezaji wa Sharia.

Mmmoja wa watuhuiwa akiwa amekatwa baadhi ya viungo vya mkono na mguu.
capitalfm.co.ke
Video ya kwanza inayoonesha waislamu wenye msimamo mkali walioteka eneo la Kaskazini nchini Mali wakiwakata viungo wanaume watano kwa tuhuma za wizi imepatikana jana Ijumaa.
Video hiyo iliyoshuhudiwa na mwandishi wa habari AFP kutoka kwa mwandishi wa Mali mjini Bamako ilipigwa na mpiga picha wa kawaida kwa makubaliano na wanajihadi, siku moja baada ya kuwakata watu hao viungo vyao chini ya sheria ya Kiislamu sharia.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, tukio hilo limetekelezwa na kundi la Movement for Oneness and Jihad in West Africa (MUJAO)ambalo limedhibiti mji wa Gao.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya