Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu UNHRC kutoa orodha ya waliotenda uhalifu wa kivita nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu UNHRC linatarajiwa kutoa orodha ya watu ambao wanatajwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kivita nchini Syria kipindi hiki ambacho vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiendelea kusonga mbele.
UNHRC imesema kutokana na vitendo vya uhalifu wa kivita kuendelea kushamiri katika nchi hiyo wanalazimika kusaka watu ambao wanajihusisha na makosa hayo kisha kuwafungulia mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.
Mkuu wa Uchunguzi kutoka Umoja wa Mataifa UN Paulo Sergio Pinheiro amesema ni wazi kwa sasa nchini Afrika Kusini kumekuwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu wa kivita ambavyo vinawalenga moja kwa moja watoto.
UNHCR kwenye mkutano wake wa ishirini na moja ndiyo wametangaza hatua ya kuwasaka wale wote ambao wamehusika na vitendo vya uhalifu ili waweze kutambulika na kisha kufikishwa ICC kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kwenye mkutano huo ambao umefanyika Geneva nchini Uswiss Shirika hilo la Kutetea Haki za Binadamu limesema litatumia video ambazo zimekuwa zikitumwa kwenye mitandao kwa ajili ya kuwabaini wale ambao wanatenda makosa hayo.
UNHCR imeweka bayana kuguswa na kitendo hicho cha kuendelea kushamiri kwa vitendo vya uhalifu wa kivita ambavyo vimekuwa chachu ya kutokea kwa mapigano kila uchao baina ya jeshi na waasi.
Shirika la Kutetea haki za Binadamu limesema mgogoro wa miezi kumi na nane nchini Syria umesababisha madhara makubwa kutokana na mapigano baina ya jeshi la serikali ya Rais Bashar Al Assad na wapinzani wake.
Takwimu za Umoja wa Mataifa UN zinaonesha watu elfu ishrini wamepoteza maisha tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria wakati Wanaharakati wakionesha takwimu zao ambazo zinataja vifo elfu ishrini na saba.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya