SUDAN - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatano 21 novemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 21 novemba 2012

Rais wa Sudani Kusini aituhumu Khartoum kutatiza uzalishaji wa mafuta

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir
REUTERS/China Daily

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema shughuli za kuanzisha tena upya uzalishaji wa mafuta zilikwamishwa na serikali ya Sudan ambayo ilileta masharti mengine mapya yahusuyo uasi uliopo katika ardhi yake.

 

Rais Kiir ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana wa mji wa Melut kunako chimbwa mafuta na kuwaambia kwamba kuchelewa huko kulitokana na vita vya huko Nil Bleu na Nouba Kordofan kusini

Rais Kiir amesema, walitakiwa kuanzisha tena shughuli hizo Novemba 15 iliopita, lakini serikali ya Karthoum ili badili msimamo na kusema kwamba bado wanakabiliana na uasi  wa monts Nouba na Bleu Nil.

Hata hivyo serikali ya Sudan imekanusha kuhusika na hatua hiyo ya kucheleweshwa kwa shughuli za uzalishaji wa mafuta ikidai kuwa pande hizo mbili zilikuwa bado hazijaafikiana kuhusu ulinzi wa mipaka baina ya pande hizo mbili wakati wa kusafirisha mafuta, ambapo ndilo sharti la kuanzishwa kwa shughuli za uchimbaji mafuta.

 

 

tags: Omar Al Bashir - Salva Kiir - Sudani Kaskazini - Sudani Kusini
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close