Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Wananchi wa Bangladesh waanza kupiga kura katika uchaguzi uliosusiwa na wapinzani

Wananchi wa Bangladesh wameanza kupiga kura hii leo katika uchaguzi ambao umesusiwa na wapinzani. Waziri Mkuu Sheikh Hasina ana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo, wapinzani wanamshutumu kiongozi huyo kupanga mikakati ya udanganyifu ili kujipati aushindi.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 150 wameuawa toka mwezi Oktoba mwaka jana baada ya Wapinzani na Wanaharakati kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo wakitaka Waziri Mkuu aondoke kwanza madarakani ili uchaguzi huo uandaliwe na taasisi huru isiyofungamana na upande wowote kisiasa.

Ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali, Wanajeshi elfu hamsini wamesambazwa katika maeneo mbalimbali licha ya ghasia kushuhudiwa hiyo jana na baadhi ya vituo vya kupigia kura kuchomwa.

Inahofiwa kuwa huenda idadi ya wapiga kura ikawa ndogo zaidi kama ilivyokuwa mwaka 1996, ambapo ni asilimia 26 pakee ya wapiga kura walijitokeza.

Wataalamu wa siasa za nchi hiyo wanaonya kuwa huenda Taifa hilo likatumbukia katika machafuko na umwagaji damu mkubwa zaidi kama ilivyoshuhudiwa mwaka 1971 wakati wa vita ya ukombozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.