Pata taarifa kuu
Misri-Kesi

Kesi ya waandishi wa habari wa kituo cha Al Jazeera nchini Misri yaahirishwa

Mkurugenzi wa Ofisi ya kituo cha Aljazeera jijini Kairo Mohamed Fadel Fahmy ameendelea kujitetea na kuomba aachiwe huru na mahakama nchini Misri inayo mtuhumu kutumia picha za video za ripoti zake bila mahusiano yoyote ya kazi yake. Reuben Lukumbuka na maelezo zaidi.

Waandishi wa habari wa Aljazeera wanaotuhumiwa kuunga mkono Muslim Brotherhood jela la Tora jini cairo on March 5, 2014.
Waandishi wa habari wa Aljazeera wanaotuhumiwa kuunga mkono Muslim Brotherhood jela la Tora jini cairo on March 5, 2014. (AFP PHOTO / KHALED DESOUKI)
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Fadel Fahmy ameripoti mahakamani alhamisi kwa mara ya tano katika kesi hiyo inayoendelea kuzua hisia kubwa katika jumuiya ya kimataifa inayo tiwa hofu na hatuwa ya kuwanyima raia haki ya kujieleza, hali inayo shuhudiwa tangu kuangushwa na jesi kwa utawala wa rais Mohamed Morsi Julay mwaka uliopita.

Katika ukumbi wa mahakama, waandishi wa habari walikuwa wameshikama pamoja na ambapo wanazuliwa jela kwa takriban siku mia moja akiwemo Peter Greste wa Australia na Baher Mohamed raia wa Misri.

Jumla ni waandishi wa habari 20 wanaoshikiliwa na mahakama nchini Misri, 12, wakihukumiwa bila kuwepo mahakamani. 16 wanatuhumiwa kuwemo katika kundi lililoitwa na serikali kuwa la kigaidi la Muslim Bradherhood huku raia wanne wa kigeni wakituhumiwa kutowa pesa vifaa na taarifa kwa ajili ya kupeperusha habari za uongo ili kuonuyesha kuwa nchini humo kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 22 mwaka huu.

Viongozi wapya wa kijeshi nchini Misri wanaendesha mapambano ya nguvu dhidi ya waandamanaji tangu Julay mwaka uliopita dhidi ya wafuasi wa rais Mohamed morsi yaliosababisha vifo vya watu 1.400 na wengine 15.000 kutowa nguvuni ambao wote ni kutika chama cha Muslim Bradherhood.

Chama hicho cha rais Morsi kilitangazwa na serikali hiyo ya kijeshi kuwa ni kundi la Kigaidi, na ambapo viongozi wake wengi wanakabiliwa na huku ya kifo katika kesi mbalimbali zinazo wakabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.