Pata taarifa kuu
RWANDA-RSF

Rwanda: Cassien Ntamuhanga atoweka katika mazingira ya kutatanisha

Mkurugenzi wa kituo cha redio cha “ Amazing Grace” nchini Rwanda ametoweka katika mazingira ya kutatanisha baada ya sherehe za kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari nchini humo.

Cléa Kahn-Sriber, mkuu wa shirika la kimataifa la wanahabari wasiyokua na mipaka “Reporters sans Frontieres” .
Cléa Kahn-Sriber, mkuu wa shirika la kimataifa la wanahabari wasiyokua na mipaka “Reporters sans Frontieres” . RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la wanahabari wasiyokua na mipaka “Reporters sans Frontieres” Cassien Ntamuhanga ametoweka wiki moja tu baada ya kituo hicho kukosoa hali ya "unyanyasaji" na " vitisho" dhidi ya waandishi wa habari vinavyotekelezwa na serikali ya Rwanda.

Ntamuhanga alisikika mara ya mwisho jumatatu jioni alipoondoka kwenye uwanja wa Amahoro wa Kigali ambapo sherehe hizo ziliadhimishwa na kutoweka ghafla na familia yake hawafamu yuko wapi.

Kulingana na vyanzo vya RSF, Ntamuhanga alihojiwa mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni na maafisa wa jeshi kitengo cha upelelezi kuhusu mmoja wa wafanyakazi wake wa zamani ambaye ameikimbia nchi ya Rwanda mwaka uliopita na kuchangia kuanzisha redio ya upinzani kwa njia ya mtandao.

Ripoti ya Taasisi ya kikamatifa inayohusika na uangalizi wa vyombo vya habari mwaka huu imeiorodhesha nchi ya Rwanda kuwa katika nafasi ya 162 kati ya nchi 180 kutokana na kuminya uhuru wa vyombo vya habari.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.