Pata taarifa kuu
EBOLA-WHO-LIBERIA-GUINEA-SIERRA LEONE-Afya

Ebola: madaktari na wauguzi wagoma Liberia

Madktari na Manesi nchini Liberia wamegoma kushinikiza serikali kuwaongezea mshahara kutokana na kuongezeka kwa kazi na hatari wanayokabiliana nayo wakati wa kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.

Homa ya Ebola imekua ni kiticho duniani, huku wauguzi na madaktari nchini Liberia wakianzisha mgomo wakiomba waongezewe mshahara kufuatia kuongezeka kwa kazi kutokana na Homa ya Ebola.
Homa ya Ebola imekua ni kiticho duniani, huku wauguzi na madaktari nchini Liberia wakianzisha mgomo wakiomba waongezewe mshahara kufuatia kuongezeka kwa kazi kutokana na Homa ya Ebola. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huu unafanyika wakati huu rais wa Marekani Barrack Obama na Francois Hollande wa Ufaransa wakisema dunia inastahili kufanya jitihada zinazo hitajika kwa kupambana na ugonjwa huu hatari.

Shirika la afya duniani WHO, limesema hadi sasa zaidi ya watu elfu nne wamepoteza maisha kutokana na Ebola na nusu ya watu hao wanatoka nchini Liberia.

Guinea na Sierra Leone ni mataifa mengine ambayo yameathiriwa na Ebola.

Mgomo wa madaktari na wauguzi Liberia
Mgomo wa madaktari na wauguzi Liberia RFI/ Olivier Rogez

Virusi vya Ebola vilienea na kushika kasi mwishoni mwaka uliyopita. Wiki hii kituo cha Marekani kinacho kagua wagonjwa kilibaini kwamba hadi mwishoni mwa mwezi wa huu wa Oktoba huenda watu 21,000 wakawa wmeaambukizwa virusi vya Ebola.

Kwa upande wake Shirika la Afya Duniani WHO limebaini kwamba hadi mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2014 huenda watu milioni 1.4 wakawa wameambukizwa ugonjwa huo, iwapo hakutofanyika jitihada za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.