Pata taarifa kuu
NIGERIA-WHO-Ebola-Afya

WHO: Nigeria yatokomeza Ebola

Shirika la Afya Duniani limetangaza rasmi Jumatatu Oktoba 20 kuwa Ebola imeangamizwa nchini Nigeria, baada ya kufanya uchunguzi wa kina.

Waziri wa Afya wa Nigeria, Onyebuchi Chukwu, akifahamisha visha vya watu 4waliobainikia kuwa na virusi vya Ebola, lakini kwa sasa Ebola imetokomezwa.
Waziri wa Afya wa Nigeria, Onyebuchi Chukwu, akifahamisha visha vya watu 4waliobainikia kuwa na virusi vya Ebola, lakini kwa sasa Ebola imetokomezwa. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Nigeria ni moja ya mataifa ya Afrika ya Magharibi yaliyokumbwa zaidi na mlipuko wa Homa ya Ebola, na kusababisha vifo vya watu wengi.

Hivi karibuni WHO ilitangaza kuwa Senegal imepiga hatua kubwa kwa kudhibiti vilivyo ugonjwa wa Ebola, na kwa sasa ugonjwa huo umeangamizwa pia nchini humo, imesema WHO.

Watu 4,500 wameuawa kutokana na Homa ya Ebola. Watu wengi miongoni mwa waliouawa kutokana na ugonjwa huo ni kutoka mataifa ya Magharibi mwa Afrika, hususan Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Hayo yanajiri wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo Jumatatu Oktoba 20 kujadili mikakati ya kudhibiti maambukizi ya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.