Pata taarifa kuu
UN-DRC-Dipolmasia

UN yaitahadharisha serikali ya DRC

Baada ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua uamzi wa kumfurusha afisa wa Umoja wa Mataifa anaehusika na haki za binadamu, Umoja wa Mataifa umeithadharisha serikali ya Congo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) akiwa pamoja na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange (kushoto),  mjini New York, Septemba 25 mwaka 2014.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) akiwa pamoja na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange (kushoto), mjini New York, Septemba 25 mwaka 2014. ©Monusco
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ameitaka serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kurejelea upya hatuwa yake ya kumfurusha jijini Kinshasa Scott Cambell, afisa wa Umoja wa Mataifa anaehusika na haki za binadamu jijini Hapo baada ya kuvikosoa vikosi vya polisi kutekeleza unyanyasaji dhidi ya raia.

Ban amesema Kutokana na hatuwa hiyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatathmini kuhusu hatuwa hiyo ya serikali ya rais Kabila.

Mbali na hayo Ban Ki Moon ameitahadharisha serikali ya Kinshasa kuendelea kuwatisha wafanyakazi wengine wa Umoja wa Mataifa jijini Kinshasa.

Kitengo cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa kimebaini katika ripoti yake kuhusu unyanyasaji uliotekelezwa na polisi katika moja ya operesheni zake za kupiga vita ujambazi kati ya mwezi Novemba mwaka 2013 na 2014 ambapo watu 9 waliuawa na wengine 32 walitoweka katika mazingira tatanishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.