Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: raia wa mashariki ya Congo waitaka Monusco kuondoka

Kumekuwa kukishuhudiwa maandamano ya wananchi mashariki mwa DRCongo tangu jumanne juma hili wananchi wakidai kuondoka kwa vikosi vya kulinda amani nchini humo Monusco.

Vikosi vya kulinda amani  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Monusco.
Vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Monusco. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Raia hao wamesema Monusco imeshindwa kuzuia kutokea kwa mauaji ya watu zaidi ya 80 katika tarafa ya Beni.

Kundi la waasi wa Uganda la ADF-Nalu lilishambulia wakaazi wa jiji la Beni katika usiku wa Octoba 15 na 16.

Baada ya mauaji hayo mkuu wa Monusco Martin Kobler ameagiza kuanzishwa haraka iwezekanavyo kwa operesheni za pamoja za vikosi vya Monusco na jeshi la FARDC kukabiliana na waasi wa ADF.

Raia wa Beni mashariki mwa Congo wakipongeza operesheni inyoendeshwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa dhidi ya waasi wa Uganda ADF-NAlu,  Machi 13 mwaka 2014.
Raia wa Beni mashariki mwa Congo wakipongeza operesheni inyoendeshwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa dhidi ya waasi wa Uganda ADF-NAlu, Machi 13 mwaka 2014. Monusco/Sylvain Liechti

Katika mji wa Mavivi kwenye umbali wa kilometa 15 kaskazini mwa jiji la Beni, ma mia ya watu wakiwemo vijana na wanawake wameandamanaJumatano Oktoba 22 wakitaka vikosi vya Monusco kuondoka kwa kile walichosema hawanamsaada wowote kwa wananchi.

Waandamanaji hao ambao walielekea kwenye makao makuu ya Monusco yaliopo karibu na uwanja wa ndege na kufaanikiwa kuvunja mlango kabla ya jeshi la Congo kuingilia kati na kuvurumisha risase hewani kuwatawanya waandamanaji hao.

Mashirika ya kiraia mashariki mwa DRCongo yanaona kuwa hii ni changamoto kubwa kwa vikosi vya Usalama nchini humo.

Hayo yakijiri tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO, imeelezea masikitiko yake kufuatia mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya makambi yake mjini Mavivi- Beni na badala yake kuwataka wananchi nchini humo kuunga mkono jitihada za Umoja huo kuhakikisha amani inarejea katika maeneo yaliyogubikwa na vita.

Hata hivyo, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Martin Kobler amekiri kwamba vikosi vya Monusco vimepoteza uaminifu kwa wananchi na kwamba lazima kurejesha imani ya umma kwa njia ya vitendo vya pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.